HabariMichezo

Wachezaji baadhi wa Ufaransa waugua ugonjwa usiojulikana

Wachezaji muhimu wa timu ya taifa ya kandanda ya Ufaransa wanaugua virusi visivyojulikana takriban saa 24 kabla ya fainali ya Kombe la Dunia.

Kocha Didier Deschamps ametatizika na uthabiti wa wachezaji muhimu wa kikosi chake.

Viungo wakabaji Raphaela Verane na Ibrahima Konate pamoja na winga Kisley Coman ni miongoni mwa wachezaji waliokosa mazoezi jana Ijumaa kutokana na ugonjwa huo.

Hii ni baada ya wachezaji Andrien Rabiot na Dayot Upamecano kukosa mechi dhidi ya Morocco kutokana na homa hiyo.

Wachezaji, wafanyakazi na vyanzo vingine vilivyo karibu na kikosi cha Ufaransa wamezungumza juu ya dalili kadhaa zinazoathiri timu katika siku za hivi karibuni ikiwa ni pamoja na homa, maumivu ya tumbo na kichwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents