Burudani

Wasanii wa mradi wa ‘Ujamaa Hip Hop Darasa’ waendelea kurekodi nyimbo kwaajili ya album ya pamoja

Wasanii wa mradi wa ‘Ujamaa Hip Hop Darasa’ ambao rapper Fareed Kubanda aka Fid Q ni mwanzilishi mwenza, wameanza kurekodi nyimbo zitakazokuwemo kwenye album yao ya pamoja.

uhhd_01-2

Akiongea na Bongo5, mmoja wa waratibu wa mradi huo unaoendeshwa kwa kushirikiana na taasisi ya Global Platform iliyo chini ya Action Aid ya Denmark, Churchill amesema mradi huo unaendelea kufanikiwa.

Churchill amesema idadi kubwa za beat zinazotumika kwenye album hiyo zimetengenezwa na vijana hao hao lakini kuboreshwa zaidi na producer mzoefu aitwaye Ben Mwamba anayeitayarisha album hiyo. Amesema darasa hilo ambalo hufanyika kila siku za Jumamosi, limekusanya vijana wa aina mbalimbali na kutoka maeneo mengi.

“Wapo wengine ambao bado wapo shule, wengi wapo katika vyuo mbalimbali na wengine wapo mtaani kwa maana kwamba wamemaliza chuo au wengine wamemaliza sekondari au shule msingi lakini wapo mtaani,” amesema Churchill.

Churchill amesema lengo la mradi huo ni kuwapa fursa vijana kukutana na kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo muziki na maisha. “Lengo hasa ni kutoa ile forum ambayo inaweza ikawaleta vijana mahali pamoja. Mbali na hip hop kuna masomo ambayo wanajifunza.”

Msikilize Churchull zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents