Michezo

Yanga yaipa somo Mtibwa Sugar, mashabiki wafurahishwa na kiwango

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kwenye mchezo huo wa kwanza kwa timu zote mbili msimu huu wa mwaka 2018/19 umeonekana kuwa wenye kasi na ufundi wa hali ya juu kwa pande zote.

Yanga imefanikiwa kupata mabao yake kupitia kwa Heritier Makambo dakika ya 31 na Kelvin Yondani akiandika la pili kupitia mkwaju wa penati dakika ya 40 wakati la Mtibwa Sugar likifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 73.

Baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani wameonekana kufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yao katika mchezo huo.

Michezo mingine iliyopigwa leo Stand United imechomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon,JKT Tanzania ikitoka sare ya 0-0 mbele ya KMC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents