Burudani

Young Killer ajibu malalamiko ya Mona G, akana kushawishiwa na watu

Baada ya producer na meneja wa Young Killer, Mona Gangster kumlalamikia kuwa anavutwa masikio na watu, rapper huyo amesema kuwa muziki wa sasa unahitaji mabadiliko makubwa.

20131223_144845
Young Killer na Mona Gangstar

Young Killer amekanusha kushawishiwa na watu kama Mona anavyoamini huku akidai kuwa suala la kurekodi katika studio zingine ni kutokana na kupata ladha tofauti.

“Mashabiki wanahitaji vitu tofauti tofauti,” Killer ameiambia Bongo5. “Halafu Mona mbona tuko naye vizuri tu! Halafu mkataba upo, sema kwamba mabadiliko ni kwamba nina uwezo wa kufanya kazi studio yoyote. Kikubwa kazi ziwe ninafanyika. Hakuna mtu ananivuta masikio. Maslahi kweli yanajulikana ni madogo, na tuNAridhika na maslahi ambayo tunayapata. Kikubwa kabisa tunahitaji kazi zifike mbali zaidi na mashabiki wanahitaji ladha tofauti,” ameongeza.

“Kwahiyo tutaendelelea kushoot video kama ile ya My Power? Unafikiri nitazishoot mpaka lini? Lazima tufanye vitu vingine vikubwa, ni lazima mabadiliko yawepo sehemu zote. Ngoma zangu zote sijui tano nimefanya pale kwahiyo ni lazima nibadilishe kuwapa ladha nyingine mashabiki wanahitaji ladha tofauti tofauti. Mona anapiga vitu vizuri lakini nimeamua kupiga na mwingine kutokana na mabadiliko ya kazi. Dear Gambe nimefanya na Mona, MrS SuperStar nimefanya na Mona, Jana na Leo nimefanya kwa Mona, My Power nimefanya kwa Mona, basi ni bora niwape ladha tofauti hata mashabiki wakisikia wanasikia kuna vitu vingine tofauti hawakuwahi kuvipata huko mwanzo. Kwahiyo tunahitaji kufika mbali zaidi. Tunahitaji kuongeza mashabiki wengi zaidi. Unajua kufanya kazi hata kwa Man Walter, Man Walter pia ana mashabiki wake na mimi nina uwezo wa kuwapata wale mashabiki, nawapataje? Ndiyo kama hivyo kufanyanao kazi. Kwahiyo tuNahitaji muziki mzuri, mabadiliko kidogo katika kazi ili tuweze kupiga hatua tusionekane tupo palepale,” amefafanua Young Killer.

Kuhusu mkataba na Mona, Young Killer amekiri ni kweli unakamilika mwezi December.

“Mkataba wetu mimi na Mona upo sawa na hakuna mapungufu makubwa, ni vitu vilevile vya kawaida vya kueleweshana vidogo vidogo ambavyo mtu yoyote anaweza akakosea na kueleweshana, ‘hapa tunatakiwa tufanya hivi tufanye hivi’. Kwahiyo ni vitu vidogo vidogo ambavyo wote tunarekebishana. Ukifika mwezi wa 12 ndipo nitakapojua niongeze au niishie hapo. Kama huko kote tumefanya vizuri mpaka hapa tulipo ina maana ni vitu vizuri. Yeye kama producer kanitangaza na mimi kama msanii nimemtangaza kama producer.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents