Burudani

Ben Pol adai alirekodi wimbo wake ‘Sophia’ bila kupanga

Ben Pol amedai kuwa ukubwa wa wimbo wake mpya, Sophia umetokana na kuimba kwa hisia pamoja na wimbo huo kuandaliwa kwa kushtukiza baada ya kuingia studio nakupenda mdundo aliokuja kuutumia kuimba wimbo huo.

10471830_1067608546598577_1170745707_n

Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa alipoingia studio kwenye shughuli zake nyingine ndipo alipokutana na mdundo wa Sophia na kuupenda.

“Niliipenda beat pamoja na tune, kwahiyo nikawa nafanya kitu ambacho nakipenda. Kwahiyo nilivyomaliza kuirekodi ndo nikaanza kuwa hii nyimbo kumbe naweza nikaitoa, wanaweza watu wakaipenda hii,” amesema Ben Pol.

“Kwasababu nilivyoingia studio sikuwa na wazo la wimbo, nimeenda studio kufanya kazi nyingine kwahiyo ndio nikakutana na hiyo beat nikiwa studio. Kwahiyo beat niliisikiliza papo kwa papo nikaipenda nikapiga freestyle, ikabidi niiandikie mzuka huwa unapotea sometimes ndo nikaandika na mambo yakatimia,” ameongeza.

Kwa upande mwingine Ben Pol amesema hadi sasa video ya Sophia imeahirishwa mara tano.

“Huwezi kuamini mpaka sasa video ya Sophia imeahirishwa mara tano kushutiwa. Lakini nataka kila kitu kiwe exclusively, kwahiyo video itafanyika na tupo kwenye process.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents