Burudani

Black wa Uswazi: Sina tatizo na Adam Juma, napenda ashoot video yangu

Rapper Black wa Uswazi amesema hawezi kugombana na Adam Juma na anapenda video yake ya ‘Kilonya’ afanye naye iwapo akikubali.

page
Rapper Black wa Uswazi na Adam Juma

Akizungumza na Daladala Beat ya Megic FM jana, Black alisema atazidi kumheshimu Adam.

“Video hii ndio maana nikasema napendaga kufanya kitu kizuri kila muda, sipendagi kufanya kitu kibaya, ndio maana najaribu bado kufikiria nitafanya na nani, lakini siwezi kusema, najaribu kuangalia nitafanya na nani video sasa hivi,” alisema.

‘Sidhani kama nitafanya na Adam Juma, lakini itavyokuwa itawezekana. Kwa upande wangu mimi Adam Juma ni mtu wangu,kwa upande wangu mimi siwezi kugombana na yule jamaa, nitazidi kum respect kama kawaida, lakini labda kwa upande wake yeye, mimi kwangu kama itakuwa poa sawa (nitafanya naYe video) mimi napenda iwe hivyo. Napenda tufanye issue za maendeleo sio za beef.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents