Soka saa 24!

Chidi Benz: Ni moyo na maamuzi yake pekee yaliyobaki kumnyanyua alikoanguka

Kuna mtaalamu wa masuala ya falsafa aliwahi kusema, ‘Yai linapopasuliwa kutoka nje huwa mwisho wa uhai kwa kiumbe kilichopo ndani,lakini yai linapojipasua kutokea ndani huwa ni mwanzo wa uhai kwa kiumbe kilichopo ndani.’

Kikubwa alichomaanisha mtaalamu huyu ilikuwa nguvu inayotoka nje bila utayari wa kutoka kwenye nafsi zetu pengine inakuwa ni kazi bure. Lakini nafsi zetu zinapoamua basi ni rahisi kwa jambo lolote kufanikiwa.
Miezi michache iliyopita rapa Chidi Benz alitoka sober alikokwenda kupata tiba baada ya kuathiriwa na madawa ya kulevya.

Babu Tale pamoja na mwanahipop na mwanaharakati anayepambana na matumizi ya dawa za kulevya Kalapina ndio waliokuwa mstari wa mbele kuona hili linatimia. Miezi michache baada ya kutoka sober na afya yake kuimarika na kuachia wimbo aliomshirikisha Ray Vanny, Chidi Benz amerudi alikotoka!!
Ni dhahiri Chidi anatumia madawa kwa mara nyingine tena ilijidhihirisha siku alipopanda kwenye jukwaa la Fiesta ya Dar na kwa clips za video zinazosambaa zikionyesha Chidi Benz akiwa amedhohofu kimwili,kiakili na kitu pekee kitakachokujulisha kuwa ni Chid Benz ni sauti yake nzito isiyo na chembe ya udhaifu!

What’s next? Maneno mengi yamesemwa na hasira za mashabiki wa Chidi Benz na muziki kwa ujumla ni dhahiri, masikitiko juu mwisho wa haya yanayotokea kwa rapa huyu ni makubwa sana,nini kifanyike na nani amsaidie rapa huyu mwenye sauti nzito,mistari kuntu,mshindi wa tunzo,na mwenye mashabiki lukuki?

Game bado inamuhitaji Chidi, Tanzania inamuhitaji, mama yake na mwanae Latifah wanamuhitaji, hakuna sober yoyote duniani inayoweza kumsaidia kuachana na madawa, hakuna mtu yeyote anayeweza kumsaidia Chidi kwa sasa.

Moyo wake ndio sober pekee inayoweza kumtoa hapa. Lazima moyo ukatae na uchukie hali aliyonayo. Lazima akubali kuwa yupo kwenye hali mbaya na anatakiwa kutoka. Akikubali pengine sober itakuwa haiitajiki tena,pengine Tale haitajiki tena. Chidi bro bado una muda na nafasi ya kurudi nafasi yako kwenye game ipo na kama mwanadamu bado unastahili kuishi.

Mungu msaidie Chidi Benz na wengine wote walio kwenye hali yake,watambue kosa walilolifanya na kurudi kwenye hali yao ya kawaida

By Eliezer Gibson ”greencity native

Phone:0769346186

Email:[email protected]

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW