Burudani ya Michezo Live

Exclusive Interview: Geez Mabovu awachana watu wanaomuongea vibaya, awaita ‘haters’ (Audio)

Geez Mabovu ni miongoni wa wasanii wakali wa Hip Hop kuwahi kutokea nchini. Anafahamika kwa sauti yake nzito na uandishi hatari wa mashairi na aliwahi kuhit na ngoma kibao ukiwemo ‘Mtoto wa Kiume’ uliotengenezwa na P-Funk Majani.

208540_465741113492582_1229885068_n
Weekend iliyopita tumekutana na rapper huyo na alikuwa na ujumbe muhimu kwa watu wanaomsema vibaya ambao anawaita ‘haters’ na kudai kuwa pamoja na muziki sasa anafanya mishemishe mingine ya kumweka mjini.

“Unaweza kukaa hapa, Mabovu amefanya vile, wao ndio watu wa kuongelea mtu tu, hao mahaters,” amesema Geez.

“Kwanini wasiongelee mambo yao binafsi? Mbona wao wapo tu wamekaa kibwege? Kwanini wasifanye mambo yao wafuatilie maisha yao? Kwahiyo Mabovu yupo, anaendelea kufanya kazi zake kwasababu kwanza hawajui hata studio nalipia shilingi ngapi ‘eti Mabovu, ngoma mpya mbona haitoki, Mabovu mbona hatukusikii? Hunisikii? wewe unapishana na media, unapishana na radio, sasa wewe unataka kuwa kama mimi tena, huwezi kuwa kama mimi, nina mambo yangu kibao, sometimes nakuwa sisikilizi radio.”

Sikiliza Interview yote hapa

Hivi karibuni Geez aliachia wimbo uitwao ‘Hawanisumbui’ aliowashirikisha Nisher na Joh Makini na ameachia pia video ya wimbo wake ‘Mateso’ aliomshirikisha Matonya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW