Michezo

Klabu ya Everton inayodhaminiwa na SportPesa yanasa kifaa kipya

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa imemsajili beki wa timu ya taifa ya Uholanzi ya vijana walio na umri wa chini ya miaka 18, Nathangelo Markelo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mchezaji wa timu taifa ya Uholanzi ya vijana walio na umri wa chini ya miaka 18, Nathangelo Markelo

Beka huyo ametua katika dimba la Goodison Park akitokea timu ya daraja la pili ya FC Volendam ya nchini Uholanzi.

Markelo ambaye anaweza kucheza nafasi ya beki wa kati ama beki wa kulia ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa anajisikia furaha kuwa mchezaji wa Everton na anajivunia kwa hilo, mipango ya klabu hiyo ni kumtumia katika kikosi cha vijana walio na umri wa chini ya miaka 23.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents