Burudani

Kuhusu King Kapita kudukua Instagram ya Linah na Joh Makini

Msanii wa Bongo Fleva, King Kapita ambaye amekuwa akiwasaidia wasanii kurudisha akaunti zao za Instagram pindi zinapodukuliwa (hack), amesema kwa sasa hivi amebadili utaratibu wa kutoa huduma hiyo kutokana na baadhi ya wasanii kuhisi yeye ndiye anafanya vitendo hivyo kwa makusudi.

Rapper huyo ameeleza hayo baada ya Joh Makini na Linah kuhisi yeye ndiye aliyedukua akaunti zao za Instagram.

“Nakumbuka akaunti ya Joh Makini mara ya kwanza kudukuliwa alinicheki nikamwambia poa nitakuchekia, uzuri yule mtu alimcheki akamtumia hela, akamrudishia akaunti yake. Alipodukuliwa mara ya pili alinipigia, Kapita rudisha akaunti yangu, hata Linah kuna kipindi alifikiri mimi ndiye niliye-hack akaunti yake, nikamwambia let do something, nenda polisi,” ameileza E-Newz ya EATV.

“Linah hackers wake wote wawili walikamatwa, mmoja alienda kuchukuliwa Sinza na mwingine Mbeya, hacker wa Joh Makini alikamatiwa Morogoro. Kwa hiyo bahati nzuri wote walikamatwa ndio maana sasa hivi nataka anayekuja kwangu kwa ajili ya msaada aende kwanza polisi awe na RB ili kulinda heshima yangu, huwezi kuwa unasaidia watu halafu unakua disrespect,” ameongeza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents