Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mourinho aeleza sababu za kuwakejeli mashabiki wa Juventus ” Walinitukana kwa muda wa dakika 90′ mimi nimewafanya kitu kimoja kidogo sana”

Mourinho aeleza sababu za kuwakejeli mashabiki wa Juventus " Walinitukana kwa muda wa dakika 90' mimi nimewafanya kitu kimoja kidogo sana"

Kocha wa Manchester United Mreno Jose Mourinho amefunguka juu ya kile kilichosemekana amewatukana mashabiki wa Juvents katika mchezo wao wa jana usiku jijini Torino.

Katika mchezo huo Manchester United walifanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo wa goli 2-1 ambayo yalifungwa na wachezaji tofauti,Juve ndio walikuwa wakwanza kufungua ukurasa wa magoli kwa goli la Cristiano Ronaldo mnamo dakika ya 65 na baada ya hapo ubao ulihamia upande wa Juve kwani mnamo dakika ya 86 ‘The supersub’ Juan Mata alipeleka zahima kwa mabibi kizee wa Torino kwa kuzamisha mpira wa freekick na kufanya matokeo yasomeke 1-1 mnamo dakika ya 88 Rashford alifanyia faulu na mmoja wa walinzi wa Juve pembezoni mwa uwanja na faulu hiyo ilikuwa kama kuwamwagia Juve maji ya moto kwani Ashely Young alifanikiwa kuipeleka faulu hiyo mahala pake na kupelekea beki wa Juve Sandro kujifunga goli hilo na ubao kubadilika na kusomeka 1-2.

Hivyo hadi mwisho wa mchezo Manchester United wakafanikiwa kuondoka na ushindi Italia ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Juventus kupoteza msimu huu lakini tangu mwaka 2009 ndio wanapoteza mchezo wa kwanza hatua ya makundi.

Baada ya kumalizika mtanange huo kocha wa Manchester Jose Mourinho kuna vitendo ambavyo alivionyesha na kuonekana kama kawatukana mashabiki wa Juve lakini Mreno huyo mwenye maneno mengi alikataa na kusema kuwa :- ” Waitaliano ni watu wazuri sana ingawa walinitukana mimi kwa muda wote wa dakika 90,mimi sikuwatukana bali niliwafanyia kitu kimoja kidogo sana, kiukweli nawaheshimu sana Juventus nawaheshimu wachezaji wa Juventus,namheshimu kocha wao, naheshimu kila kitu hapa nimefurahishwa sana na vijana wangu kwa kweli wamejitahidi wameonyesha kiwango kizuri ”

Mchezo ulikuwa mzuri sana mchezo wa viwango vya juu,mchezo ulikuwa wa kiwango cha juu zaidi nahis tumecheza kwa kiwango cha juu zaidi,baada ya goli lao niliona kama tuna dakika 5 za kucheza lakini timu ilifanya hivyo kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho”

“Juventus wana wachezaji wa wachezaji bora sana,Goli la Cristiano Ronaldo lilikuwa bora sana na Leonardo Bonucci alitoa pasi nzuri sana akiwa kama beki wa kati nahisi wana wachezaji bora zaidi pia rekodi bora kabisa katika uwanja wa nyumbani, tumebakisha mchezo mmoja nyumbani wa kucheza na Young boys kama mahesabu yangu yataenda vizuri basi tutafuzu hatua inayofuata endapo Valencia hawatoifunga Juventus nahisi kwa sasa tuwaachie watu wa Old Trafford nafikiri tulifika mapema niwashukuru Polisi wa hapa kwa escort yao tumaini langu tunaweza kupata alama zingine tatu”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW