Burudani

Mr. Flavour wa Naija akanusha tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mshindi wa BBA 2013 Dillish Mathews

Zile tetesi zilizokuwa zimesambaa katika mitandao mbalimbali siku za hivi karibuni kuwa kuna dalili za kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya star wa Nigeria Flavour na mshindi wa BBA mwaka jana (Tha Chase) Dillish hatimaye zimepata majibu.

dillish n flv

Hit maker wa ‘Ashawo’ Flavour Nabania amekanusha tetesi hizo na kusema Dillish Mathews wa Namibia siyo mpenzi wake.

“Kwa sasa hakuna kitu kati yetu”, Alisema Flavour “yeye(Dillish) alishiriki katika video yangu na mimi nilienda kumpokea uwanja wa ndege na pia kuwa mwenyeji wake. Ni Hivyo tu. Nashangaa kwanini wanaeneza uongo mtandaoni, sisi si watoto na kama kuna kitu kati ya yetu kwa nini tufiche? Kwa sasa ni kikazi zaidi”. Hayo ni maelezo ya Flavour katika exclusive Interview na jarida la burudani Encomium la Nigeria wiki iliyopita.

flavour-2

Tetesi za wawili hao kuwa wapenzi zilianza kusambaa baada ya picha walizopiga pamoja zikiwaonesha wakiwa karibu zaidi ya kawaida kusambaa hivi karibuni.

Kingine kilichochochea tetesi hizo ni baada ya Dillish na aliyekuwa boyfriend wake kuachana siku chache zilizopita na kufanya watu waamini wameachana sababu ya Flavour.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents