Burudani

Peter Okoye wa P-Square apata dili zito Marekani

Peter Okoye maarufu kama Mr P, kutoka kundi la P-Square amesaini mkataba na kampuni ya usambazaji wa muziki ya Empire kutoka Marekani.


Msanii Peter akisaini mkataba na kampuni ya Empire

Neema hiyo imemdondokea msanii huyo baada ya hivi karibuni kuibuka kwa tetesi za kuvunjika kwa mara ya pili kwa kundi lao la muziki ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu walipoliunda tena baada ya kuvunjika mwaka jana.


Peter akiwa na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Empire

Msanii huyo ameonyesha kufurahia hatua hiyo kwa kuandika kwenye mtandao wake wa Instagram, “Thank you Lord??? RepostBy @empire: “Just had a digital distribution deal with @peterpsquare! Welcome to the #EMPIRE family!” (via #WhizRepost @AppsKottage).”

Kampuni ya Empire ambayo makao yake makuu ni San Franciscomjini California, inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Kendrick Lamar pamoja na makampuni mengine makubwa duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents