Tia Kitu. Pata Vituuz!

Queen Darlin amsupport Diamond kuhusu msimamo dhidi ya baba yao

Dada yake na mwanamuziki wa Bongo Flava aliyefanikiwa sana Diamond Platnumz, Queen Darlin ameibuka na kumuunga mkono kaka yake huyo kwa kutojali maneno ya baba yao kuwa hawamjali.
Kupitia magazeti ya udaku wiki iliyopita baba yake mzazi na Diamond alidai kuwa mwanae Diamond amemtenga na wala hamjali.
Alidai kuwa hamsaidii kama anavyofanya kwa mama yake na pia simu zake hazipokei.
Queen Darlin naye amesema baba yao huyo alimtosa pia kipindi alipokuwa mdogo kiasi cha kushindwa hata kuwafahamu baba zake wadogo.
Akihojiwa na Clouds Fm, Diamond alielezea sababu ya yeye kumpotezea baba yake ni kutokana na kumtelekeza na hivyo kulelewa na mama yake zaidi.
“Inamaana ananijua mimi mwanae baada ya kujua mimi nimekua Diamond, siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angekaa angenisomesha angenipa elimu nzuri, lakini siku zote nilihangaika na mama yangu mzazi na ndo maana siku zote mama yangu mzazi kipaumbele.
“Nisingependa kusikia mtu yoyote anadiriki kuzungumza kwamba mimi ndo baba yake, wasitake kuonekana kipindi cha maslahi mtu ndo anajifanya yeye ndo anahusika sana na mimi kama mtoto wake, sipendi.”
Mi nimeanza kusema tangu natoa wimbo wa binadamu, nasema upendo popote, ulipo kwa baba yangu (anaimba) japo alinikataa, katika wimbo wa binadamu hata sijui kama leo ntakuja kuwa na Prado. Hata kabla ya kuwa hivi niliimba before kabisa, sina mbele sina nyuma, ina maana nisionekane na thamani mtoto wa fulani sasa hivi, kwasababu nimekuwa fulani, hapana wasinitengenezae mazingira mbaya mbele ya wananchi.
Mzazi wangu ataendelea kuwa baba yangu tu, lakini asifikiri kupata priority kama anayopata mama yangu kwasababu angetaka hiyo angeonesha kunijali na kunithanimi mapema kama mzazi.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW