Tupo Nawe

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatano hii, Rashford, Alderweireld, Conte, Bale, Oblak, Herrera, Hazard, Rodriguez na wengine sokoni

Mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford, 21, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa thamani ya pauni milioni 78. (Mirror). United inapania kuanzisha mchakato wa usajili wa mlinzi wa Ubelgiji Toby Alderweireld kwa pauni milioni 25 kutoka Tottenham. Bado haijawasiliana na Spurs kuhusina na kiungo huyo wa miaka. (Sun)

Meneja wa zamni wa Chelsea mtaliano Antonio Conte, 49, yuko tayari kujiunga na Inter Milan kama meneja wao mpya – ikiwa klabu hiyo itamfanya kuwa meneja anaelipwa kitita kikubwa zaidi katika ligi ya Serie A. (Mail)

Antonio Conte
Image captionMeneja wa zamAni wa Chelsea mtaliano Antonio Conte

Ajenti wa Gareth Bale, anasema kiungo huyo wa kimataifa wa Wales wa miaka 29, anafurahia uwepo wake Real Madrid na kwamba winga huyo hana mpango wa kurudi katika ligi ya Premia. (Mirror)

Atletico Madrid inaazimia kutoa ofa mpya kwa kipa Jan Oblak. Kiungo huyo wa kimataifa wa Slovenia, 26, pia ametajwa kuwa katika orodha Manchester United kuchukua nafasi ya David de Gea. (Marca)

Kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach, Thorgan Hazard, 26, anaazimia kusalia katika ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga ili apate nafasi ya kujiunga na Borussia Dortmund.

Hata hivyo klabu yake ya sasa ina mpago wa kumuuza kwa Liverpool baada ya klabu hiyo ya ligi kuu ya England kuzidisha ofa ya euro milioni 42 iliyotolewa na Dortmund. (Nieuwsblad – in Dutch)

Thorgan Hazard
Image captionThorgan Hazard

Kiungo wa kati wa Uhispania Ander Herrera, 29, anakagua ofa za timu nyingine na bado hajatia saini mkataba mpya Manchester United kwasababu ”hajaafikiana” na klabu hiyo. (ABC – in Spanish)

Vilabu vya Arsenal na Tottenham vinapania kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan Croatia Ivan Perisic, 30. (Corriere dello Sport, via Sport Witness)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Mcolombia James Rodriguez, 27, anatarajiwa kuhamia Juventus huku Eden Hazard, 28, akisubiriwa kutua katika uwanja wa Bernabeu. (Marca)

James Rodriguez
Image captionJames Rodriguez

Hazard hatatia saini Chelsea, hata ikiwa klabu hiyo itamua kuzinguana na Real. (Telegraph)

Liverpool huenda ikampoteza kiungo wa kati Mreno Rafael Camacho msimu huu baada ya mazungumzo ya mkataba wake kukwama. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, amesema kuwa ataendelea kuichezea Crystal Palace, licha ya tetesi kuibuka kuwa huenda akarejea Manchester United. (Manchester Evening News)

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW