Diamond Platnumz

Ziara ya Diamond barani Ulaya kumuingizia takriban shilingi milioni 100

Hivi karibuni Diamond Platnumz alilazimika kuahirisha ziara yake ya barani Ulaya baada ya waandaaji kushindwa kukamilisha kumlipa hela yake ya advance katika muda muafaka.

diamond

Inadaiwa kuwa katika ziara hiyo Diamond alitakiwa kulipwa dola 50,000 ambazo ni takriban shilingi milioni 80 za Kitanzania na ameithibitishia Bongo5 kuwa ni kweli japo kuna taarifa kuwa kiasi hicho alikikataa.

Ameiambia Bongo5 kuwa ziara hiyo itafanyika mwezi ujao ambapo baada ya ziara hiyo atarudi nyumbani na kisha kwenda tena kwaajili ya nyingine. Kutokana na makubaliano mapya ya ziara hiyo kuna uwezekano wa ziara hiyo ya kwanza kumuingizia karibu shilingi milioni 100 ama zaidi.

Jumamosi hii Diamond alilazimika kutumia website yake kutoa taarifa ya kuahirisha kwa ziara hiyo.

“Kutokana na kampuni ya United Events Ltd Tilburg-The Netherlands kwa upande mwingine kama promoter kushindwa kutimiza baadhi ya mahitaji ikiwemo kushindwa kulipa pesa ya show ambayo ilitakiwa ifanyike Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/Germany 09/03/2013 na zingine kama East African Night ambayo ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/Holland tarehe 15/03/2013 na kadhalika, mimi na team yangu nzima ya wasafi hatutoweza kuhudhuria kwenye events hizo,” alisema.

“Nilikuwa nikipata maswali mengi sana toka kwa mashabiki zangu mbalimbali wakiniuliza kuhusiana na ujio wangu wa nchi hizo za EUROPE lakini siku zote nilikua kimya sikuweza kujibu wala kuzungumza chochote na wadau wangu kutokana na kutokuwa na uhakika wa tour hiyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents