Diamond Platnumz
Prokoto ya Victoria Kimani f/ Diamond & Ommy Dimpoz yatajwa kuwania tuzo za Nigeria
Wimbo wa msanii wa Kenya, Victoria Kimani ‘Prokoto’ aliowashirikisha Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz umetajwa kuwania tuzo za ELOY (Exquisite Lady Of The Year) za nchini Nigeria.
Wimbo huo ulitayarishwa na Tudd Thomas. Tuzo hizo huandaliwa na jarida la EXQUISITE.
Tuzo za ELOY zilianzishwa kwa madhumuni ya kuwatambua wanawake na kazi zao katika fani mbalimbali nchini Nigeria.
Kimani ametajwa kuwania kipengele cha Female Music Artist ambapo anachuana na wasanii nguli wa Nigeria wakiwemo Chidnma, Waje, Tiwa Savage, Yemi Alade, Emma Nyra na wengine.