Hello! Grace Matata na Maua sama kuachia wimbo wao wa pamoja December hii
Muimbaji Grace Matata amepotea sana kwenye muziki toka awe mama, lakini haimaanishi kuwa ameacha kufanya muziki kwani anatarajiwa kusikika tena kwenye wimbo mpya alioshirikiana na msanii mwenzake wa kike Maua Sama.
Grace Matata na Maua Sama ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Mucobbs kilichoko Moshi wamekutana kwenye collabo waliyoipa jina la ‘Hello’.
Maua na Grace
Kupitia akaunti zao za Instagram Grace na Maua wameshare taarifa za ujio wa collabo yao.
“I know its been a LONG time! This December……..” ameandika Grace Matata.
Na Maua ameandika “Another hit song #KUBWAKULIKO Coming soon! Me an my grace on dis one! ! this December kaeni mkao wa kula its #Hello @Mauasama and @gracematata @ematheboy #keepingthegoodmusicAlive.”
Kwenye post nyingine Maua ameandika, “#Halo amazing song! ! Classic vocals from me @Mauasama and my grl @gracematata early this December! ! Ya’all need to here it
Its the continuation of gud music! ! #Hello #HELLO #HALLO #HALLO #HALLO”.
Rapper Fid Q ameufananisha muungano wao wa collabo kama wa Beyonce na Rihanna, kwenye moja ya comments Fid ameandika:
“Hatari..!! Yaani hiyo ni sawa na Beyonce akifanya collabo na Rihana..”