Burudani
Muongozaji wa filamu ya Straight Outta Compton F. Gary Gray kuingoza Furious 8
Muongozaji wa filamu ya Straight Outta Compton, F. Gary Gray ataiongoza filamu ya Furious 8.
Muigizaji wa filamu hiyo, Vin Diesel alipost picha Facebook akiwa na muongozaji huyo.
Mtandao Deadline.com umeripoti kuwa wawili hao walifanya mkutano na kufikia makubaliano hayo. Gray alisemekana kuwa chaguo la kwanza la kampuni ya Universal.
Sio jambo la kushangaza kwakuwa filamu yake ya Straight Outta Compton imeingiza zaidi ya dola milioni 200.