Michezo
Robson-Kanu wa Wales aingia kwenye 18 ya Lionel Messi
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Wales na klabu ya West Bromwich Albion ya Uingereza, Robson-Kanu amefanikiwa kuingia kwenye vita ya kuwania tuzo ya goli bora kwa mwaka 2016 maarufu kama Puskas Awards akiungana na wachezaji wengine 10 akiwemo Lionel Messi.
Robson-Kanu amefanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo kutokana na goli alilolifunga kwenye robo fainali ya kombe la Euro dhidi ya Ubelgiji mwezi Juni mwaka huu.
Wachezaji wengine waliotangazwa kuwania tuzo hiyo ni: Mario Gaspar (Spain), Hlompho Kekana (South Africa), Marlone (Brazil), Lionel Messi (Argentina), Neymar (Brazil), Saul Niguez (Spain), Daniuska Rodriguez (Venezuela), Simon Skrabb (Finland) na Mohd Faiz Subri (Malaysia).