Habari

Rwanda yashtumiwa kupanga shambulizi la kutaka kumuua msaidizi wa Pierre Nkurunziza

Nchi ya Burundi imeishutumu Rwanda kwa madai ya kupanga kufanya majaribio ya kutaka kumuua msaidizi wa Rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe.

250bb942-e85d-4c6d-a438-ec5ec9f78cb7_mw1024_mh1024_s

Msemaji wa jeshi la polisi kutoka Burundi, Pierre Nkurukiye amesema maagizo ya kufanywa kwa jaribio hilo lililofeli, yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa wapangaji waliotoka kwenye jeshi la Burundi.

Nyamitwe alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko Burundi lakini si mara ya kwanza kupatwa na tukio kama hilo. Mwezi Julai mwaka huu Burundi iliishtumu Rwanda kwa mauaji ya Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Hafsa Mossi aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents