Michezo

Debuchy ampa wasiwasi Arsene Wenger

Mchezaji wa klabu ya Arsenal Mathieu Debuchy kuna wasiwasi kwamba jeraha alilolipata siku ya Jumapili ni baya, kocha Arsene Wenger amesema.

_92685283_debuchy_getty

Debuchy, 31, ambaye alicheza kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2015 mechi ya Ligi ya Premia dhidi ya Bournemouth ambayo walishinda 3-1 lakini akaumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka uwanjani baada ya dakika 16.

“Itanibidini kuzungumza na matabibu, lakini unaweza tu kujua hali halisi baada ya saa 48,” alisema Wenger.

“Unahitajika kuacha damu itoke kisha baadaye tuwe na uchunguzi wa MRI baada ya saa 48 kubaini ubaya wa jeraha.”

Magoli ya Arsenal katika mechi hiyo yalifungwa na Alexis Sanchez mabao mawili na moja la Theo Walcott.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents