Habari

Raia wa Gambia kuchagua wabunge leo

Kwa mara ya kwanza wananchi wa Gambia wanafanya uchaguzi wao wa kwanza wa kuchagua wa bunge leo (Alhamisi).

Hii ni mara ya kwanza kwa raia hao wa nchi hiyo kufanya uchaguzi huo tangu rais wao wa zamani Yahaya Jammeh alipoondolewa kwenye kiti hicho baada ya utawala wake wa miaka 22. Chini ya utawala wa Barrow bunge la nchi hiyo ndio litakuwa na jukumu kubwa la kutunga sheria tofauti na utawala wa rais aliyepita [Yahaya Jemmah] ambaye alikuwa akitunga sheria zake binafsi na kulipuuza bunge.

Wananchi wa Gambia wamekuwa na imani kubwa na rais wao mpya baada ya kuwajumuisha wakuu wa vyama saba tofauti vya kisiasa ambao waligombea katika uchaguzi mkuu uliopita.

Nacho chama cha APRC kilichokuwa kinamuunga mkono Yahaya Jammeh pia kimepata muwakilishi katika baraza hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents