SportPesa wamkabidhi Waziri Mwakyembe Milioni 50 za Serengeti Boys (Video+Picha)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh Dk Harrison Mwakyembe leo amekabidhiwa hundi ya kitita cha Shilingi milioni 50 na Kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo ya SportPesa ili kusiaidia timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys.
Waziri Mwakyembe wakati wa makabidhiano hayo amesema ameishukuru sana kampuni hiyo na kuahidi kuwa Serikali kupitia wizara yake itashirikiana na kampuni ya SportPesa ili kuweza kukuza michezo hapa nchini.
“Kutokana na kutokuwa na mfumo mahususi wa kupata pesa ndiyo maana tunachangisha niwashukuru sana Abbas Tarimba ambae ni Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania na napenda niwahakikishie kuwa Wizara itashirikiana na nyie“Amesema Waziri Mwakyembe.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Bw Abbas Tarimbo amesema wametoa fedha hizo ili kuonyesha watanzania kuwa ni kwa kiasi gani kuwa kampuni yao imejikita zaidi kunyanyua Soka la Tanzania.
SportPesa tayari wapo kwenye mazungumzo ya mwisho kumalizana na Vilabu vya Yanga na Simba SC ili kukamilisha mikataba ya kudhamini Klabu hizo kongwe nchini Tanzania.
By Godfrey Mgallah