Burudani

Angelina Jolie aonesha jeuri ya pesa

Mwigizaji wa filamu Angelina Jolie, ameamua kuonesha jeuri ya pesa kwa kununua mjengo mpya wakisasa zaidi uliupo jijini Los Angles.


Angelina Jolie

Jolie mwenye umri wa miaka 41 amenunua nyumba yenye thamani ya dola milioni 25 ikiwa ni miezi minane tangu kuachana na mume wake mwigizaji wa filamu, Brad Pitt.

Nyumba hiyo ni miongoni mwa nyumba zenye mvuto katika jiji hilo, ina ukubwa wa mita za mraba 7,500, ipo maeneo ambayo wasanii wengi maarufu wanaishi akiwemo Casey Affleck, Natalie Portman, Lauren Graham, Will.I.Am na David Fincher.

Angelina na Brad wana watoto sita ambao ni Maddox, Pax, Zahara, Shiloh, Knox na Vivienne, kati yao wapo aliowaasili.

Mwaka 2004 Jolie na Brad Pitt walianza mahusuano na ilipofika mwaka 2014 walifunga ndoa. Wawili hao mwaka jana waliachana.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents