Burudani

P the MC achomoa ishu ya Wakazi na Godzilla

Rapper P the MC amekataa kuzungumzia kiundani ‘beef’ kati ya msanii wa kundi lao ‘Sisi Sio Kundi (SSK)’, Wakazi na Godzilla kwa kusema walishajitambulisha wao sio kundi hivyo suala hilo haliigusi SSK.

P the MC ameeleza  suala hilo halihusiani na SSK linapaswa kuchukuliwa kama la Wakazi ila wanapoona kuna sehemu anaenda sivyo wanakaa na kushauriana nae.

“Kwanza watu wanatakiwa wafahamu sisi sio kundi, kwa hiyo yule ni Wakazi sio SSK, kwa hiyo Wakazi ana mipaka yake na anaweza kufanya vitu ambavyo hata sisi pengine tusivipende lakini kwa sababu yeye anavipenda na kwa vile sisi sio kundi anaruhusiwa kuvifanya,” P the MC amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha E FM.

“Vikipitiliza huwa tunakaa chini na kumuambia dah!, Wakazi hii ishie hapa achana nayo, tena na kweli anatusikiliza kwa sababu ni washikaji zake yanaisha,” ameongeza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents