Burudani

Video: Huwa siamini figisu figisu – Alikiba

Msanii wa muziki Bongo Flava, Alikiba amesema haamini figisu figisu katika muziki bali ni kufanya kazi nzuri tu.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ‘Seduce Me’ ameiambia Bongo kuwa kufanya muziki mzuri ndio njia pekee yake ya msanii kufika mbali na si vinginevyo.

“Kwa upande wa figisu figisu huwa sielwi na sina uhakika lakini what I know imeandikwa kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake, ni kutokana na kazi yako na juhudi yako, utafika pale unapotakiwa kufika na hiyo inatokana na jinsi na wewe unafanya muziki wako,” amesema Alikiba.

“Huwa siamini figisu figisu, kuna kipindi maneno fulani yalisikika kwamba Alikiba hawezi kutoboa bila featuring na wasanii wa Nigeria, lakini hapana, mimi nilipenya mwenyewe, nilifanya wimbo pekee yangu akapenya na ukapendwa,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents