Burudani

Kylie Jenner na Travis Scott wanatarajia kupata mtoto

Mrembo kutoka familia ya Kardashian, Kylie Jenner na mpenzi wake Travis Scott wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeripoti kuwa Kylie aliwapa taarifa za ujauzito huo marafiki zake mapema mwezi huu katika tamasha la Day N Night Festival lililofanyika Anaheim, California.


Picha mpya ya Kylie Jenner akiwa na marafiki zake

Wakati huo huo chanzo hiko kimeuambia mtandao huo kuwa Travis na yeye amewapa taarifa hizo watu wake wa karibu.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo anatarajiwa kuzaliwa mwezi February mwakani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents