Saba saba 2008 ulinzi mkali

Jeshi la Polisi na mgambo wameanza kutumika kwa pamoja katika kusaidia ulinzi ndani ya viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere Jijini, ikiwa ni hatua mojawapo ya Halmashauri ya Biashara ya Nje, BET katika kuimarisha usalama wa watu na mali.

Jeshi la Polisi na mgambo wameanza kutumika kwa pamoja katika kusaidia ulinzi ndani ya viwanja vya maonyesho vya Mwalimu Nyerere Jijini, ikiwa ni hatua mojawapo ya Halmashauri ya Biashara ya Nje, BET katika kuimarisha usalama wa watu na mali.

Mkurugenzi wa BET, Bw. Ramadhan Khalfan, amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kupambana na wimbi la vibaka ambao huvamia katika viwanja hivyo wakati wa maonyesho. Akasema tofauti na mwaka jana ambapo kazi hiyo walipewa makampuni binafsi ya ulinzi.

“Hofu ya kuwepo vibaka haipo tena… washiriki na watembeleaji wasiwe na hofu kwani Jeshi la Polisi na mgambo wako pamoja katika kuwadhibiti” akasema Bw. Khalfan.

Alasiri ilipotembelea katika viwanja hivyo, ilishuhudia mgambo pamoja na askari wakivinjari katika maeneo mbalimbali ndani ya uwanja huo. Wakati huo huo, wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya Panasonic wameiomba Serikali kudhibiti wimbi la bidhaa bandia nchini.

Mkurugenzi wa Clock Tower Shopping Center, Bw. Khalid Salim amesema wimbi hilo limekuwa likiwaingizia hasara wananchi kwa kuwa bidhaa hizo hazidumu.

“Kampuni ya Panasonic inafanya mapinduzi kila mara kukabiliana na ushindani wa kibiashara, lakini tatizo la bidhaa bandia nalo limekuwa likisababisha hasara kwa wananchi” alisema.

Akasema kampuni yake ambayo imeshika nafasi ya kwanza katika kundi la wauzaji wa bidhaa za umeme kwenye maonyesho hayo, wamekua wakitoa garantii ya mwaka mmoja kwa kila bidhaa watakayouza.

Akasema jambo hilo limesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta imani kwa wananchi kuhusiana na uhalisi wa mtengenezaji.

Akawashauri wananchi kununua bidhaa kutoka kwa wakala wa kampuni hiyo ili kuepuka kuingizwa katika mtego wa wauzaji wa bidhaa bandia nchini. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa kampuni hiyo kunyakua ushindi wa kwanza katika kundi la bidhaa za umeme baada ya kushiriki katika maonyesho hayo kwa miaka mitano.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents