Habari

Serikali kudhibiti umiliki wa laini za simu, ukitaka ya pili utaomba TCRA

Serikali imesema itaanza kudhibiti umiliki holela wa laini za simu na hivyo chini ya usajili wa laini kwa alama za vidole mtu akitaka kusajili laini zaidi ya mbili itabidi ajaze fomu ya kueleza kwa nini anataka laini ya pili.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye aliyeeleza kuwa katika udhibiti huo watashirikiana na NIDA kupitia vitambulisho vya Taifa.

Amesema kuwa mtu akitaka kusajili laini ya pili ya simu Kampuni za simu zitamuona na kujua kuwa tayari ana laini ya kwanza, hivyo lazima atajaza fomu maalum kueleza kwa nini anataka laini ya pili.

Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha ‘line’ za simu zitaanza kuuzwa kwenye maduka rasmi na mtu anayesajili atachukuliwa alama za vidole na picha yake.

Serikali imesema itaanza kudhibiti umiliki holela wa laini za simu na hivyo chini ya usajili wa laini kwa alama za vidole mtu akitaka kusajili laini zaidi ya mbili itabidi ajaze fomu ya kueleza kwa nini anataka laini ya pili.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye aliyeeleza kuwa katika udhibiti huo watashirikiana na NIDA kupitia vitambulisho vya Taifa.

Amesema kuwa mtu akitaka kusajili ‘line’ya pili ya simu Kampuni za simu zitamuona na kujua kuwa tayari ana ‘line’ ya kwanza, hivyo lazima atajaza fomu maalum kueleza kwa nini anataka ‘line’ ya pili.

Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha ‘line’ za simu zitaanza kuuzwa kwenye maduka rasmi na mtu anayesajili atachukuliwa alama za vidole na picha yake

Related Articles

19 Comments

  1. Kwaiyo nikitaka lain ya TTCL ( rudi nyumbani kumenoga! kama kauli mbiu yao inavosema) itabidi niombe tcra,nani atakua anapoteza mda wake huo? Kwa msingi huo ttcl ambao hakuwepo kwenye soko la ushindani mda mrefu wata struggle kupata wateja

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents