Mrembo Vera Sidika atangaza kuachana na Mpenzi wake Otile Brown atoa sababu hizi
Mrembo Vera Sidika atangaza kuachana na Mpenzi wake Otile Brown atoa sababu hizi
Mrembo na mwanamitindo kutoka nchini Kenya Vera Sidika ameamua kuweka hadharani sababu zilizopelekea kuachana na mpenzi wake ambaye ni mwanamziki Otile Brown.
Vera Sidika amekuwa mtu maarufu sana kutokana na kazi yake ya Uanamitindo pia akifungua ofisi inayohusiana na mambo ya Urembo Jijini Nairobi nchini Kenya.
Mapenzi yao yamedumu kwa zaidi ya miezi miatu hadi hivi sasa na mwishowe Mrembo huyo ameamua kuweka wazi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa mapenzi yao yamefikia mwisho.
Vera ameweka wazi kuwa amechoshwa na matendo ambayo anafanyiwa na mwenza wake kwani kabla ya kutoka kwa video ya ngoma ya Otile inayokwenda kwa jina la Baby Love ambayo yeye Vera ametumika kama Video Queen kuwa hampendi.
Penzi lao lilikuwa limegubikwa na maneno mengi sana wengi wakionekana kumshauri Otile kuachana na Vera kwani hawaendani lakini pia kabla ya kutoka video ya Baby Love ambayo ni ngoma ya Otile ilisemekana wameachana lakini kumbe ilikuwa kiki ya wimbo huo
Sidika ameongea mengi sana katika waraka aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram.
soma hapa
By Ally Juma.
Zilikuwa kiki ! Za nyimbo
mpeni namba zangu… mi natafuta mke
Kashindwa mikito
Kumewachea hivyo tena, bila kiki nacskendo hampat tonge cjui nyie watu
Anataka sifa tu mbona mie nilipo muacha sikumtangazia
Vyombo vya plastiki havidumu