Uongozi Simba Wamtaka Mziray

Uongozi wa klabu ya Simba umeanza mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Syllersaid Mziray `Super Coach` kwa ajili ya kuingia mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali inayoshiriki.

Uongozi wa klabu ya Simba umeanza mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Syllersaid Mziray `Super Coach` kwa ajili ya kuingia mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali inayoshiriki.

Uongozi huo umefikia maamuzi hayo baada ya kumalizana na kocha wake kutoka Bulgaria, Krasimir Bezinski, ambaye ameshindwa kuipa mafanikio timu hiyo katika mechi zake za Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kumalizika mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 14.

Akizungumza na Nipashe mmoja wa viongozi wa Simba alisema kuwa tayari wameshaanza mazungumzo na Mziray na hatua iliyofikia ni kukubaliana na dau ambalo kocha huyo analitaka ili asaini mkataba.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa mbali na mazungumzo na Mziray pia wanatarajia kuwa na kocha mwingine kwa ajili ya kuliboresha benchi la ufundi la timu hiyo.

“Tunatarajia kukamilishana naye mazungumzo wakati wowote, leo anatarajia kuzungumza naye � kwa ajili ya kukubaliana kiasi cha fedha za mshahara � atakachokuwa anapata,“ alisema kiongozi huyo.

Aliongeza kuwa kocha huyo, ambaye ni mwalimu katika Chuo Kikuu Huria amesema kuwa anataka kulipwa kiwango kisichotofautiana sana na kile alichokuwa analipwa Kocha Bezinski.

Nipashe ilipowasiliana na Mziray alikanusha kufanya mazungumzo na uongozi wa Simba na kuongeza kuwa mambo yatakapokuwa tayari yatawekwa wazi.

“Hakuna kitu kama hicho, ni uvumi tu na maneno ya watu,“ alisema Mziray.

Kocha huyo aliitwa katika benchi la ufundi la Simba kama mshauri hivi karibuni wakati timu hiyo ilipokuwa inajiandaa kucheza na watani zao, Yanga hivi karibuni.

Kocha mwingine, ambaye anadaiwa kufuatwa na viongozi wa Simba ni Mkenya, Jacob Mulee na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Twalib Hilal aliyeko Oman huku Abdallah Kibadeni akiwatolea nje na kuwataka viongozi wajipange kwanza.

Simba imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa katika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kutokana na kujikusanyia jumla ya pointi 14.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents