Muziki
Mfahamu mkali wa afrobeat kutoka Nigeria mwenye makazi yake Sweden ‘Anthony Sky’ (+ Video)
Anthony Sky ni msanii wa kimataifa wa afro pop, afrobeat, mwimbaji / mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Nigeria lakini makazi yake kwa sasa yakiwa Stockholm Sweden.
Kwa sasa akiwa amesainiwa chini ya Real Definition Music iliyopo nchini Uingereza 🇬🇧.
Mnamo tarehe 26 Machi 2021 ataachia album yake ya “LOUDA” na pia katika album hiyo akiwa amewashirikisha wasanii wawili wa Tanzania, ambapo itakuwa inapatikana kupitia YouTube, Spotify, boomplaymusic, Audiomack na nyingine.
Anthony Sky anawaomba Watanzania Wanigeria na mataifa yote yatakayoupenda muziki wake kumpa sapoti kwenye kazi zake.
Hii ni moja ya ngoma zake inayoitwa “Balancia”
Tuambie unampa asilimia ngapi Anthony Sky kwa dude hili,,,…! Dondosha comment yako hapa chini.