Habari
Tetemeko la ardhi laitikisa Ugiriki
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha richter limekumba eneo la kati mwa Ugiriki leo na kuwalazimu wakazi katika mji wa Larisssa kukimbilia barabarani.
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 katika kipimo cha richter limekumba eneo la kati mwa Ugiriki leo na kuwalazimu wakazi katika mji wa Larisssa kukimbilia barabarani.
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Jiologia la Marekani. Taasisi ya masuala ya jiologia mjini Athens, imesema kuwa kitovu cha tetemeko hilo ambalo lilisikika katika maeneo ya kati na kaskazini mwa Ugiriki ni umbali wa kilomita 21 Kusini mwa mji wa Elassona karibu na Larissa.
Hakukuwa na ripoti za mara moja kuhusu majeruhi. Hata hivyo, maafisa katika eneo hilo wameripoti kuhusu uharibifu wa majengo hasa yale ya zamani ambapo aidha kuta zake ziliporomoka ama kupata ufa.