Habari

Ufaransa, Ujerumani na Uhispania kuunda ndege ya pamoja ya kivita

Ujerumani, Ufaransa na Uhispania zimesema leo kwamba zimekubaliana kuhusu hatua zitakazofuata za kutengeneza aina mpya ya ndege ya kivita.

Huo ndio utakuwa mradi mkubwa zaidi wa ulinzi barani Ulaya na utagharimu zaidi ya Euro bilioni 100 ambayo ni sawa na dola bilioni 121.4.

Ufaransa hasa imegharamia mradi wa utengenezaji wa ndege ya kivita itakayojumuisha mifumo ya kizazi kipya ya kurusha ndege bila rubani, na imesema ni muhimu katika ulinzi wa kujitegemea hasa mnamo wakati kuna ushindani kutoka China, Urusi na Marekani.

Hatua itakayofuata katika mradi huo wa mfumo wa kivita wa angani (FCAS) inatarajiwa kugharimu euro bilioni 3.5. Fedha ambazo zitatolewa na Ufaransa, Ujerumani na Uhispania kwa kiwango sawa.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba nchi hizo zinajenga moja kati ya ala muhimu zaidi kwa ulinzi wa mataifa yao katika karne ya 21.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents