HabariSiasa

Waandamana kupinga ugumu wa maisha Liberia

Watu zaidi ya alfu moja nchini Liberia walishiriki katika maandamano kupinga ugumu wa maisha.

Watu hao pia wanapinga rais wao George Weah kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu.

Maandamano ya mara kwa mara yamefanyika katika uongozi wa miaka mitano wa rais huyo na ghadhabu imeongezeka jinsi serikali yake inavyosimamia uchumi wa nchi.

Bei za chakula na nishati zimepanda kutokana na athari za janga la corona na vita vya nchini Ukraine.

Maandamano yaliyofanyika kwenye mji mkuu wa Liberia, Monrovia yaliandaliwa na vyama vikubwa vinne vya upinzani.

Weah amekuwa nje ya nchi tangu mwishoni mwa Oktoba, wakati huo aliitembelea Qatar kumwangalia mwanawe, Timothy Weah, aliyechezea timu ya Marekani katika Kombe la Dunia na pia alihudhuria mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika mjini Washington. Anatarajiwa kurudi Liberia Jumatatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents