Afisa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries, Emila Tom Machuve (kulia) akizungumza na mmoja wawashindi wa promosheni ya bia ya Pilsner ijulikanayo kama‘Kapu la Wana’ wakati wa droo ya tatu ya promosheni hiyoiliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwakilishikutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgufi akisimamia mchakato huo. Kwenye droo hiyo, walipatikana washindi saba kutoka kanda ya Ziwa, Kusini naKaskazini ambapo promosheni ya Kapu la Wana inafanyika.