Burudani

Disi la Ze Dudu

Ze Dudu

The Bongo Hip Hop Legend, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amezindua harakati mpya ya kuitetea Hip Hop na Bongo Flava pamoja na wasanii wake kwa kutoa CD inayoelezea kinagaubaga unyonyaji unaoendelea aliyoipa jina la Nguruwe.

In that CD, Ze Dudu a.k.a Baba Willy anawachana presenters & DJ’s ambao wanatajwa kuishi kimjini kimjini kwa mgongo wa wasanii ambao wanawanyonya.

Mbali na kuwadisi presenters & DJ’s hao, pia Dudu ametoa shut out kwa waandishi na wadau wa burudani Bongo kama Saleh Ally wa Championi, Amour Hassan wa The Guardian, Fina Mango, Masoud Kipanya, MC George na Abby Cool wa Global Publishers na wengine wachache ambao wanaheshimu taaluma kwa kutokuendekeza rushwa.

Kwa sauti kavu, pia Dudu amewagonga nyundo baadhi ya wana Hip Hop wanaojiita wanaharakati kwamba sifa hiyo haiendani nao kwa sababu ni wanyonge na hawajui kutetea haki.

“Mimi kuna ma-DJ wamegoma kupiga nyimbo zangu tangu mwaka 2006, miaka minne bado nipo. Sijaenda kuomba msamaha na ninaishi, sisi ndiyo ma-legendary wa huu muziki, tumetoka nao mbali halafu watu wanakuja kula kiulaini.

“Mtu unaimba Hip Hop unajiita mwanaharakati, siku mbili nyimbo zako hazichezwi redioni unakwenda kuomba msamaha, unapiga magoti, siku mbili!” Ze Dudu anasikika akigonga sauti ndani ya CD hiyo.

Akichambua umafia wa baadhi ya watangazaji na ma-DJ Bongo, Ze Dudu anamwaga kuwa kuna watu wameweka mkakati kwamba bila shilingi 500,000 hawaruhusu kupiga nyimbo redioni kitu ambacho ni sawa na unyonyaji.

“Hizo laki tano tano msanii atatoa kwa redio ngapi? Kwa uwezo upi? Halafu unatengeneza albamu kwa milioni 4, unakwenda kwa mdosi unalipwa milioni 2, msanii atapata nini?” Anahoji Ze Dudu na kuongeza:

“Mtangazaji anakupigia simu anakuuliza upo wapi? Unamjibu upo baa, baada ya dakika chache anakuja na wapambe, demu wake, wanaagiza vinywaji vya bei mbaya eti ‘bili’ yote juu yako msanii. Watu tuna familia, mimi mwanangu Willy anasoma International School.”

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents