Burudani
Pweza Paul afariki
Pweza Paul, almaarufu kama ‘The Oracle’, aliyekuwa mtabiri mahiri amefariki pande za Ujerumani katika Sea-Life Center jijini Oberhausen.
Paul alijipatia umaarufu duniani kote kwa kutabiri kwa usahihi mechi 8 za Kombe la Dunia 2010 na pia kuitabiria timu ya Spain kutwaa Kombe la Dunia.
Paul alikuwa ametimiza muda wa pweza kuishi miaka 2 na nusu na hivyo kufa kwenye tank lake asubuhi ya Jumanne.
Inasemekana Paul alikufa kifo cha kawaida tu kwa kuwa muda wake wa kuishi ulishapita.