Super Shine kuzindua albamu mbili Navy Beach
Kundi la muziki wa taarafu nchini la Super Shine linaloongozwa na Salma Yahaya ‘Queen Salm’. Akizungumza na Bongo5, alisema hivi sasa wanajiandaa na uzinduzi wa albamu mbili kwa wakati mmoja.
Alisema albamu yao ya kwanza inanyimbo nne, na ya pili ina nyimbo tano zote watazindua kwa pamoja kwakuwa yakwanza ilichelewa kuzinduliwa. Pia ameongeza kwa kusema kwamba uzinduzi wa albamu zote hizo, zitafanywa siku ya juma pili Navy Beach.
Alisema Bonanza hilo litaitwa Marafiki wa ukweli, familia na uzinduzi wa albamu mpya.
Pia alisisitiza katika uzinduzi huo, ambao pia nyimbo mbili mpya zitazindulishwa ikiwemo Proffesional Love ulioimbwa na Hasssan Zumo na Red Card uliyimbwa na Rahma Yahaya. katika uzinduzi huo utasindikizwa na ‘KHANGA MOJA, ndembendembe,Jokha Khasim na Hassan Ally.
Nuru Njama, mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo.
Nuru Njama mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo.
Rahma Yahaya mwimbaji wabendi hiyo
Kiongozi wa bendi ya Super Shine Queen Salma ‘Salma Yahaya’
Mtoto wa bendi ya Super Shine Baby Chammy.