Burudani

Asia wa ‘Leo’ atengeneza app ya simu ili kuwawezesha mashabiki kupata muziki wake kwa urahisi

Msanii wa muziki anayetamba na wimbo wa ‘Leo’ Asia Mjun ametengeneza app yake binafsi ‘Asia Mjun’ itayowawezesha mashabiki wa muziki wake kupata muziki wake kwa urahisi.

Asia-Cover

Akizungumza jana na radio Free Africa, Asia amesema hii itawasaidia mashabiki wake kupata kazi zake pamoja na profile yake ya muziki.

“Mimi kama msanii wa kwanza naweza nikasema hivyo najivunia kuwa na app, kwa sababu inarahisisha kupatikana kwa kazi zangu kwa urahisi, show zangu kazi zangu zote, kila kitu changu, ukihitaji kujua unaweza uka download app ukaona kazi zangu, kuna nyimbo yangu ya kwanza Mtoto wa Mjini, kuna nyimbo yangu ya pili inaitwa Nawaumbua nimefanya na Shilole na kuna nyimbo yangu ya tatu ambayo sasa hivi inafanya vizuri inaitwa Leo, hizo nyimbo zote zina video zake na unaweza ukazipata huko,” alisema Asia.

Screenshot_2014-11-11-17-39-25

Katika hatua nyingine meneja wa Asia, amesema hii ni njia itafanya msanii huyo kuwa na mashabiki wake karibu.

“Asia pia anafanya na movie ukiingia kwenye app utaona akaunti zake mbalimbali, hii nimefanya hivi kwajili ya kumtangaza na kumtengeneza mapema kuanzia huku chini, nakujua kuna wasanii wakubwa hawana App ya simu kwa Tanzania, ukitaka ku-download nyimbo unaweza, kusikiliza, unaweza ukasikiliza palepale pia utakuta video zake, licha ya kuwarahisishia mashabiki kupata kazi za Asia, pia ni njia ya kumpata msanii kwa urahisi, kama kuna mtu au kampuni anataka kufanya kazi na Asia itakuwa rahisi kufuatilia profile yake kwa sababu ndani App ya Asia Mjun utakuta kila kitu unachohitaji, hii App imetengenezwa na Musa kutoka KINU.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents