Ben Pol mpaka Egypt kwenye World Youth Forum

Staa wa muziki wa R’nB kutoka Tanzania, @iambenpol awa miongoni mwa mastaa wachache watakaoshiriki jukwaa kubwa zaidi la vijana duniani #WorldYouthForum (@wyfegypt) linalotarajiwa kufanyika Jijini Sharm El Sheikh, nchini Egypt Januari 10- 13, 2022.

Ben Pol ataambatana na Mastaa wengine kama Inspector Murillo (Raquel Murillo) wa Spain aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia series ya Money Heist, Muigizaji na mchekeshaji Anwar (America) na wengine.

World Youth Forum ilianzishwa mwaka 2017 nchini Egypt na kuzinduliwa na Rais wa nchi hiyo Abdel Fattah Al-Sisi, na kila mwaka hukutanisha vijana kutoka kila pembe ya dunia kuhamasisha Amani, Ustawi, Umoja na Maendeleo kwa dunia nzima.

Related Articles

Back to top button