Burudani

Club Bilicanas kusherekea miaka 20 na street bash!


Club maarufu ya usiku Afrika Mashariki na kati, Club Billicanas kesho inatimiza miaka 20 tangu kufunguliwa kwa mara ya kwanza chini ya jina hilo hilo mwaka 1992. Kwa mujibu wa mmoja wa wahusika katika klabu hiyo ya usiku, klabu hiyo imeamua kufanya sherehe za kutimiza miaka hiyo 20 sambamba na kituo cha Radio Clouds Fm ambao nao wanatimiza miaka 13 wikiendi hii.

Kabla ya kufunguliwa upya na kupewa jina hilo la Club Billicanas, kiota hicho kilikuwa kinaitwa Mbowe Club kwani kinamilikiwa na Mbunge wa jimbo la Hai na Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe.

Tayari shamra shamra za shrerehe hizo zimeshaanza ambapo Club Billicanas na Clouds Fm wamekandaa Street Bash, katika eneo la maegesho ya magari ambapo kutakuwa na jukwaa na Screen kubwa ambapo wasanii watatoa burudani huku ma DJ wakikupigia nyimbo kwa mtindo wa video na audio.

Bongo5 inapenda kuipongeza menejimenti na uongozi wa Club billicanas kwa ujumla kwa kutimiza miongo miwili ya kuwapa watanzania na wageni burudani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents