Burudani

Chris Brown apigwa chini na girlfriend wake baada ya kuenea kwa taarifa kuwa ana mtoto na msichana mwingine

Girlfriend wa muimbaji Chris Brown, Karrueche Tran ameamua kuchukua uamuzi wa kujiweka pembeni baada ya kufahamu kuwa boyfriend wake ni baba wa mtoto wa miezi tisa.

Tran n Brown

TMZ iliripoti kuwa Chris Brown alimzalisha model wa zamani aitwaye Nia, ambaye hata Karrueche alikuwa anamfahamu na waliwahi kula bata pamoja lakini hakujua kama amezaa na Breezy.

Karrueche ambaye hana muda mrefu sana toka arudiane na Breezy waliyeachana miezi kadhaa iliyopita, ameshindwa kuvumilia na kuutangazia ulimwengu uamuzi alioamua kuuchukua baada ya kufahamu uwepo wa kiumbe chenye damu ya boyfriend wake.

Kupitia Twitter Karrueche ameandika:
“Listen. One can only take so much. The best of luck to Chris and his family. No baby drama for me.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents