Burudani

Chris Brown atoa remix ya ‘Somebody Else’ je amemuimba Riri?

Toka mkali wa R&B Chris Brown aachane na Rihanna kumejitokeza vitu vingi vinavyoashiria kuwa wapenzi hawa wa zamani wanatumiana ujumbe usio wa moja kwa moja kupitia njia tofauti.

chris-brown2

Baada ya Rihanna kutweet ujumbe ulioonekana dhahiri unamhusu Breezy kwa kumuita “Queen” siku tatu zilizopita, Chris naye ametoa remix ya wimbo wa Mario unaoitwa ‘Somebody Else, wenye maneno yanayoshabihiana na matatizo kati yake na Riri.

Katika wimbo huo uliotengenezwa na producer Polow Da Don, Chris amemuimba msichana ambaye amemsaliti na kufall in love na mtu mwingine “Somebody” else.

Breezy anategemea kutoa album yake mpya ya “X” (July 16) mwaka huu.

Isikilize hapa “Somebody Else” ya Chris.

Kama hukuwai kuisikia original version ya Mario isikilize hapa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents