Burudani

Deepika Padukone: Fedha na mafanikio sio vitu muhimu maishani

Muigizaji wa Bollywood, Deepika Padukone amesema anaamini katika maisha fedha na mafanikio sio vitu muhimu.

ei-208837

“Kukubalika ni muhimu. Tunafanya kazi ili iweje? Kama nikifanya kazi kwa bidii kwa filamu zangu na kama kazi zangu hazikubaliki, sasa nini maana yake,” Deepika Padukone alisema kwenye mahojiano.

“Kiukweli, fedha ni kitu cha mwisho na pia mafanikio sio muhimu. Kupendwa na kukubalika ndio kitu muhimu na cha thamani zaidi.”

Muigizaji huyo ameigiza kwenye filamu nyingi za Bollywood kama “Cocktail”, “Yeh Jawaani Hai Deewani”, “Chennai Express” na “Goliyon Ki Raasleela Ram-leela”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents