Habari

Dkt. Jakaya Kikwete akutana na Rais Magufuli Ikulu, mwenyewe aeleza kilichompeleka (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Leo tarehe 23 Oktoba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kikwete na Rais Magufuli

Baada ya mazungumzo hayo,  Dkt. Kikwete amesema wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu.

Nimekuja kumsalimia nakumtakia kila la heri, anafanya kazi nzuri, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote ya kumpa nguvu, tupo tayari kumsaidia,”amesema Mhe. Rais Mstaafu Kikwete.

Aidha, Mhe. Rais Mstaafu Kikwete amebainisha kuwa Mhe. Rais Magufuli anafanya kazi nzuri na amemtaka aendelee hivyo hivyo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents