Burudani

Exclusive: AT kuvunja ukimya kwa kuachia video ‘matata’ ya ‘Kitumbua’

Baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu, mfalme wa mduara, AT anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao Kitumbua.

2

4

Kwa muda AT alikuwa Oman alikokwenda kupumzisha akili na kuwafuata mashabiki wake wa huko ili kuweza kujua nini wanahitaji kutoka kwake huko anasema alipata mapokezi mazuri na kukutana na watu tofauti walioahidi
kumsaidia kufikia malengo.

Akiongelea jinsi alivyojipanga baada ya kimya chake, AT ameiambia Bongo5, “Kikubwa nikuwaonesha kuwa nipo na jamii kuwaamsha kujua walitoka wapi na wapi wanatakiwa kuenda kupitia njia tofauti ya elimu kinachofuata ni ile burudani nzuri itakayomvutia kila mmoja wetu nakuweza kuwakilisha TZ katika ramani nyingine kupitia
milango tofauti.”

3
AT akiwa katika pozi za video

Ameongeza, wimbo mpya ni KITUMBUA ambao katika video zote hii itakua kivutio kwa kila mtu sababu ipo tofauti na video zote za mduara pia imebeba watu wakubwa ambao majina yao yameshatangulia kimataifa
kama Cholo Ganun ambae alisha mpigia Ganun Mwanamuziki wa marekani kwajina ni John Legend ambae alionesha dunia ustadi wa kazi yake katika wimbo wa Show me uliofanyika Zanzibar.”

5

Hata mtoto aliyecheza humo ni Mzanzibar ambaye naye ni mlezi wa mwanamuziki huyo kwa sasa pia kuna mpiga Violin na Tab ambao wataonekana humo ni watu wazito na kimuziki ila kama haitoshi AT atakua amevalia Kifalme pia atakuwa ni mtu wa pili ukimtoa Mfalme wa kwanza kutawala Zanzibar Said bin Said kuivaa Hanjur, wengine wanaita Jambia wengine wanaita Upanga wa kuvalia tumboni.

1
Mfalme wa kwanza kutawala Zanzibar Said bin Said

Hanjar hiyo ina umri wa miaka 400 ambayo imehifadhiwa
MTONI PALACE kwaajili ya kumbukumbu video hiyo Imefanywa na Kampuni ya KWETU STUDIO inatarajiwa kutoka wiki hii panapo Majaaliwa.!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents