Diamond Platnumz

Exclusive Audio: Diamond aeleza sababu ya kutohudhuria KTMA jana + kuwashukuru mashabiki

Hitmaker Diamond Platnumz jana hakuweza kuhudhuria tuzo za Kili licha ya kushinda tuzo mbili kubwa zilizopokelewa na watu wengine kwa niaba yake. Diamond amezungumza na Bongo5 kueleza sababu iliyomsababisha ashindwe kwenda kupokea tuzo zake mwenyewe.

IMG_8903

Amesema alishindwa kwenda kwenye kilele cha tuzo hizo kubwa nchini zilizotolewa jana kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwakuwa alitakiwa kwenda kwenye uzinduzi wa kinywaji kipya cha kampuni ni ya Cocacola, kiitwacho Novida uliofanyika jana usiku kwenye mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Golden Jubelee, jijini Dar.

IMG_8820

Amesema akiwa kama balozi wa Cocacola ilikuwa ni lazima ahudhuria uzinduzi huo. Diamond alishinda tuzo mbili ikiwemo kubwa ya msanii bora wa kiume.Msikilize zaidi hapa ambapo anawashukuru pia waliompigia kura.

Picha: This is Diamond

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents