Afya

Fahamu umuhimu wa mafuta ya nazi kiafya

Mafuta ya nazi ni fatuta ambayo hutokana na nazi, na hapa utengenezwa kwa kukuna nazi, kisha kukamua tui zito na baadae kulipika tui hilo hadi kugeuka kuwa mafuta.

1. Husaidia afya ya Moyo

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa ajili afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.

2. Huongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.

3. Huongeza nguvu mwilini

Ni chanzo kizuri cha nguvu mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo susafiri moja kwa moja hadi kwenye ini na hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’.

4. Mubadala ya kupikia

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, pia ni mazuri kwa wasiopenda mafuta ya wanyama. Kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

5. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu

Mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli za ubongo na katika kusaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

6. Husaidia katika ugonjwa wa aleji

Moja wapo ya faida ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.

Zingatia:
Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, Ila ni vizuri kuyatengeneza mwenyewe ilikuepuka kuchanganyiwa na kemikali nyingine na kama unapikia kwenye chakula chenye nazi kama wali usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

Chanzo:Dk Fadhili Paulo

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents